Signed in as:
filler@godaddy.com
The New York Tanzanian Community is a 501(c)(3) non-profit organization registered in the great state of New York.
Ndugu WanaJumuiya,
Uongozi unapenda kuwashirikisha kwenye Muhtasari wa yaliyojiri kwenye Kikao chake na Kamati ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kutathimini Ufanisi wa Utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika Alhamis Juni 8, 2023 kwenye Ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu Umoja wa Mafaifa.
Muhtasari huu wenye kurasa tano (5) unaweza kusomwa moja kwa moja kwenye website yetu au kwa kupakua (download) na kuusoma offline kwa kubonyeza PAKUA MUHTASARI hapo chini.
Ahsanteni,
Uongozi NYTC
Wajumbe wa Kamati ya kufanya tathmini ufanisi wa Utendaji Kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, iliyoteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, inategemea kuwa na mkutano wa kukusanya maoni na Viongozi wa jumiya za Watanzania (Diaspora) siku ya Alhamisi, Juni 8, 2023, ndani ya ukumbi mikutano za ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania, Umoja wa Mataifa.
Ajenda kuu za mkutano zitakuwa kama zifuatazo:
1. Ushirikiano wa Diaspora na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
2. Mchango wa Dispora katika ujenzi wa diplomasia ya kiuchumi
Wanajumuiya wanahimizwa kuwasilisha maoni yao kupitia viongozi wa jumuiya kupitia group la WhatsApp la Jumuiya, kwa email ya jumuiya info@nytanzaniancommunity.org au kupitia fomu (Bonyeza kitufe cha Wasilisha Maoni yako Hapa ) iliyoambatanishwa na Tangazo hili.
Maoni yatakusanywa kuanzia leo Jumatatu, Juni 5, hadi siku ya Jumatano Juni 7, 2023.
Ahsanteni,
Imetolewa na Ungozi NYTC
Updates Juni 8, 2023: Muda wa kukusanya Maoni Umeshapita. Fomu ya kuwasililsha maoni imeondolewa.
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya WaTanzania New York City na Viunga vyake, Bw. Nathan Chiume, kwa mashauriano na Bodi ya Wadhamini (Board of Trustees), na Kwa matakwa ya Katiba ya Jumuiya Sehemu ya 3.6 inayompa mamlaka ya kuziba nafasi za wazi kwenye Uongozi wa Kamati Tendaji (Executive Committee), ameteua Viongozi wapya wafuatao:
1. Dk. Mwemezi Basil Deusdedit kuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya
2. Dk. Nyemo Mbennah kuwa Naibu Mweka Hazina wa Jumuiya
Aidha, kulingana na Katiba ya Jumuiya sehemu ya 3.10 (m,n,o) inayompa mamlaka Mwenyekiti wa Jumuiya kuteua wajumbe au Kamati Maalum ya kusaidiana na Kamati Tendaji, amemteua
1. Mhandisi Kinyasi Monyi kuwa Mkuu wa Masuala ya Teknolojia ya Jumuiya.
Uteuzi huu unaanza rasmi Mei 30, 2023.
Dr. Mwemezi Basil Deusdedit - Secretary
Dr. Nyemo Mbennah - Deputy Treasurer
Eng. Kinyasi Monyi - Chief Technology Officer
Mr. Nathan Chiume - Chairperson
Mr. Gaston Mkapa - Deputy Chairperson
Ms. Victoria Mwanyonga - Deputy Secretary
Mr. Sam Mfalila - Treasurer
**The board of trustees has suspended the requirements for active membership (Yearly fees) in this election cycle**
We are dedicated to improving the lives of those in our community. Your contribution today helps us make a difference.
Copyright © 2023 New York Tanzanian Community - All Rights Reserved.