New York Tanzanian Community
  • Home
  • About Us
    • Our Mission
    • NYTC Constitution
    • Executive Committee
    • Board of Trustees
    • Financial Reports
  • Membership
  • Programs
  • Events
  • Archives
    • 2023
    • 2022
    • 2021
    • 2020
    • 2019
  • More
    • Home
    • About Us
      • Our Mission
      • NYTC Constitution
      • Executive Committee
      • Board of Trustees
      • Financial Reports
    • Membership
    • Programs
    • Events
    • Archives
      • 2023
      • 2022
      • 2021
      • 2020
      • 2019
New York Tanzanian Community
  • Home
  • About Us
    • Our Mission
    • NYTC Constitution
    • Executive Committee
    • Board of Trustees
    • Financial Reports
  • Membership
  • Programs
  • Events
  • Archives
    • 2023
    • 2022
    • 2021
    • 2020
    • 2019

Welcome to New York Tanzanian Community

Welcome to New York Tanzanian CommunityWelcome to New York Tanzanian CommunityWelcome to New York Tanzanian Community

The New York Tanzanian Community is a 501(c)(3) non-profit organization registered in the great state of New York.

A Night of Hope & Togetherness, AGM & Election Day

Ndugu Wanajumuiya,


Tunazidi kuwaomba kwa unyenyekevu kuendelea kuchangia kufanikisha shughuli yetu ya Jumamosi, December 6, 2025. Zaidi ya kuchagua viongozi wapya wa Executive, pia tutaadhimisha miaka 64 ya Uhuru wa Tanganyika, pamoja na kusherehekea mwisho wa mwaka 2025 kwa vyakula, vinywaji, na muziki.


Taarifa zaidi:


  1. Mgeni Rasmi atakuwa Mlezi wa Jumuiya yetu, Balozi Dr. Suleiman Haji Suleiman, Kaimu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
  2. Ni ruksa kutoa mchango kadiri ya uwezo wako. Kushindwa kutoa mchango haimaanishi hauruhusiwi kuhudhuria kwa sababu huu ni mkutano wa Uchaguzi, na tungependa wanajumuiya wengi washiriki.
  3. Hata hivyo, gharama za shughuli hii ni kubwa, na wote tunafahamu kwamba mfuko wa Jumuiya hauwezi kukidhi gharama zote. Gharama ya mtu mmoja tu sio chini ya $80.
  4. Hivyo basi, mchango-elekezi (suggested donation) kwa kila mmoja wenu tunaomba usiwe chini ya $80 kama ikiwezekana.
  5. Watoto chini ya umri wa miaka 18 watangia bure. Tukiweza wote kutoa suggested donation hapo juu, tunaamini tutaweza ku-cover gharama za watoto wetu.


TAFADHALI TUMA MCHANGO WAKO WA KUFANIKISHA SHUGHULI HII KUPITIA:

(A) ZELLE ACCOUNT YA JUMUIYA YETU:
ZELLE ID: NYTC COMMUNITY EMAIL:
info@nytanzaniancommunity.org

(B) CASHAPP: TO NYTC TREASURER, DR. NYEMO MBENNAH, PHONE 651-706-3995. Tafadhali weka jina lako kamili kwenye Memo section.

TUNATANGULIZA SHUKRANI ZETU KWENU🙏🏿

Asanteni sana!


UONGOZI - NYTC Executive

NYTC Summer BBQ announcement

Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania NY, NJ, CT na PA (NYTC) unawakaribisha wanajumuiya wote kwenye BBQ kali ya mwaka! Watoto, ndugu, jamaa na marafiki pia wanakaribishwa. 


Kutakuwa na Muziki kutoka kwa DJ wakali DJ Mao na DJ Richard, Michezo ya watoto, Nyama Choma, Vinywaji, after BBQ party, na kadhalika.  Pia tutakuwa na fursa ya kuwasikiliza Viongozi wetu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Jumuiya yetu, hususani suala la mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba na usajili mpya wa wanachama. 


Mgeni rasmi siku hiyo anatarajiwa kuwa Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Balozi Hussein Kattanga. 


Kama ilivyo ada, ukiwa kama mwanajumuiya tunaomba Support yako ya mchango ili kufanikisha shughuli yetu. Wachangiaji wote watapewa Wristbands maalum watakazozivaa mkononi wakati wote ili kupata huduma na kutambua juhudi zao za kufanikisha shughuli yetu, ambayo pia ina lengo la kutunisha mfuko wa Jumuiya. Suggested donation ni $100 kwa familia.


Tafadhali tuma mchango wako kwa Kinyasi Monyi kupitia:

  • Zelle - 585-642-8633
  • Ca$happ $kinyasi
  • Venmo - @kinyasi22


Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na:

  1. M/KATIBU, Dada Victoria (443-557-8034) au
  2. Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Dada Zelda (917-912-3479)!


Soma Flyer iliyoambatana na hili tangazo au BOFYA HAPA kwa Taarifa zaidi kuhusu Siku, Muda, na Mahali itakapofanyika BBQ yetu.


Karibuni nyote!


IMETOLEWA NA;

UONGOZI-NYTC

JULY 10, 2024

TAARIFA KWA WANAJUMUIYA NEW YORK TANZANIAN COMMUNITY!

NYTC Community Virtual Townhall Meeting

Ndugu Wanajumuiya, 


Uongozi wa Jumuiya unapenda kuwakaribisha kwenye mkutano wa Wanajumuiya na Viongozi wake utakaofanyika siku ya Jumapili, June 9, 2024 kuanzia saa 1 kamili Usiku (7:00pm) hadi saa 3 kamili usiku (9:00pm). kwa njia ya Zoom.


Mkutano wetu utakuwa na agenda zifuatazo:


1. Utambulisho mwingine wa Viongozi wa Jumuiya na wajumbe wa Kamati za Jumuiya.

2. Kutoa Mapendekezo na kupokea Maoni kuhusu Mabadiliko ya vifungu vya Katiba kuhusu masharti ya Uanachama na benefits za uanachama, kabla ya kuwasilishwa kwa Bodi kwa ajili ya utekelezaji.

3. Kuanza kwa mchakato wa Usajili wa wanachama wapya na wa zamani kupitia database kwenye website yetu.

4. Kuanzishwa kwa Program za Ushirikiano (Partnerships) zenye manufaa (benefits) kwa wanachama walialipa ada za uanachama.

5. Mkakati wa kuhimiza wanachama kujiunga na program za kusaidia kipindi cha misiba, na ushirikishwaji wa viongozi wa jumuiya pale misiba inapotokea.

6. Kalenda ya Sherehe za Jumuiya kwa mwaka mzima, pamoja na kuanzishwa kwa “Quarterly Zoom Town Halls.”

7. Mengineyo.


Unaweza kujiunga Mkutanoni kupitia Zoom kwa kubobyeza link hii: https://tinyurl.com/NYTC-Zoom-meeting


Meeting ID: 848 2697 9824

Passcode: Wasiliana na Uongozi kupitia group la Jumuiya Whatsapp.  


Ahsanteni,


Uongozi - NYTC


06/052024

Muhtasari Kikao cha viongozi jumuiya na kamati ya mhe. RAis

Ndugu WanaJumuiya,


Uongozi unapenda kuwashirikisha kwenye Muhtasari wa yaliyojiri kwenye Kikao chake na Kamati ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kutathimini Ufanisi wa Utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika Alhamis Juni 8, 2023 kwenye Ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu Umoja wa Mafaifa.


Muhtasari huu wenye kurasa tano (5) unaweza kusomwa moja kwa moja kwenye website yetu au kwa kupakua (download) na kuusoma offline kwa kubonyeza PAKUA MUHTASARI hapo chini.


Ahsanteni,


Uongozi NYTC

PAKUA MUHTASARI

KAMATI YA RAIS JUU YA TATHIMINI MAMBO YA NJE YAINGIA NYC

Wajumbe wa Kamati  ya kufanya tathmini ufanisi wa Utendaji Kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, iliyoteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, inategemea kuwa na mkutano wa kukusanya maoni na Viongozi wa jumiya za Watanzania (Diaspora) siku ya Alhamisi, Juni 8, 2023, ndani ya ukumbi mikutano za ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania, Umoja wa Mataifa.


Ajenda kuu za mkutano zitakuwa kama zifuatazo:


1. Ushirikiano wa Diaspora na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

2. Mchango wa Dispora katika ujenzi wa diplomasia ya kiuchumi


Wanajumuiya wanahimizwa kuwasilisha maoni yao kupitia viongozi wa jumuiya kupitia group la WhatsApp la Jumuiya, kwa email ya jumuiya info@nytanzaniancommunity.org au kupitia fomu (Bonyeza kitufe  cha Wasilisha Maoni yako Hapa ) iliyoambatanishwa na Tangazo hili.


Maoni yatakusanywa kuanzia leo Jumatatu, Juni 5, hadi siku ya Jumatano Juni 7, 2023.


Ahsanteni,


Imetolewa na Ungozi NYTC


Updates Juni 8, 2023: Muda wa kukusanya Maoni Umeshapita. Fomu ya kuwasililsha maoni imeondolewa.

Uteuzi

Taarifa kwa WanaJumuiya

Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya WaTanzania New York City na Viunga vyake, Bw. Nathan Chiume, kwa mashauriano na Bodi ya Wadhamini (Board of Trustees), na Kwa matakwa ya Katiba ya Jumuiya Sehemu ya 3.6 inayompa mamlaka ya kuziba nafasi za wazi kwenye Uongozi wa Kamati Tendaji (Executive Committee), ameteua Viongozi wapya wafuatao:


1. Dk. Mwemezi Basil Deusdedit kuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya

2. Dk. Nyemo Mbennah kuwa Naibu Mweka Hazina wa Jumuiya


Aidha, kulingana na Katiba ya Jumuiya sehemu ya 3.10 (m,n,o) inayompa mamlaka Mwenyekiti wa Jumuiya kuteua wajumbe au Kamati Maalum ya kusaidiana na Kamati Tendaji, amemteua


1. Mhandisi Kinyasi Monyi kuwa Mkuu wa Masuala ya Teknolojia ya Jumuiya.


Uteuzi huu unaanza rasmi Mei 30, 2023.

Dr. Mwemezi Basil Deusdedit - Secretary 

Dr. Nyemo Mbennah - Deputy Treasurer

Eng. Kinyasi Monyi - Chief Technology Officer

Jumuiya ya WaTZ NYC & Viunga Vyake Yapata Viongozi Wapya

Mr. Nathan Chiume - Chairperson

Mr. Gaston Mkapa - Deputy Chairperson

Ms. Victoria Mwanyonga - Deputy Secretary

Mr. Sam Mfalila - Treasurer

Tangazo la Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya ya NYTC

Sifa za Wagombea

  1. Awe Mtanzania (au nasaba ya Utanzania) kwa kuzaliwa, kuoana na mtu Mwenyezi nasaba ya Tanzania au naturalized citizen.
  2. Awe mkazi wa kuthibitishwa wa NYTC (NY, NJ, CT & PA)
  3. Akubaliane na kufuata Kanuni na taratibu za NYTC
  4. Awe hajawahi kushika nafasi anayogombea kwa zaidi ya miaka minne (4) hapo nyuma
  5. Awe na umri zaidi ya miaka 18
  6. Awe hajahukumiwa na makosa ya jinai 
  7. Awe hajajihusisha na makundi ya kigaidi 
  8. Awe hajajihusisha na matukio ya kihalifu 

Sifa za Mpiga Kura

  1. Awe Mtanzania (au nasaba ya Utanzania) kwa kuzaliwa, kuoana na mtu mwenye nasaba ya Tanzania au naturalized citizen.
  2. Awe mkazi wa kuthibitishwa wa NYTC (NY, NJ, CT & PA)
  3. Akubaliane na kufuata Kanuni na taratibu za NYTC 
  4. Awe na umri zaidi ya miaka 18

**The board of trustees has suspended the requirements for active membership (Yearly fees) in this election cycle**

Bofya Hapa kupakua fomu ya kugombea Uongozi NYTC
Bofya hapa kujisajili kupiga kura Uchaguzi NYTC 2023

Help your community, donate now!

$0.00
Pay with PayPal or a debit/credit card

We are dedicated to improving the lives of those in our community. Your contribution today helps us make a difference.

Tanzania in News

Our Supporters

  • Home
  • Our Mission
  • NYTC Constitution
  • Executive Committee
  • Board of Trustees
  • Financial Reports
  • Programs
  • Events
  • Contact Us
  • 2023

Copyright © 2026 New York Tanzanian Community - All Rights Reserved.

Powered by

This website uses cookies.

We use cookies to analyze website traffic and optimize your website experience. By accepting our use of cookies, your data will be aggregated with all other user data.

DeclineAccept